Wednesday, 30 October 2013

BREAKING NEWS: MWANAMKE MMOJA APIGWA RISASI TRA JIJINI ARUSHA

Mwanamke mmoja amepigwa risasi ya mkononi kutokana na uzembe wake mwenyewe.

Mwanamke huyo alifika maeneo ya TRA ambako kuna tawi la CRDB - Mapato na kupaki gari eneo lisiloruhusiwa. Askari walimuelekeza eneo hilo haliruhusi kupaki gari lakini alikataa na kuingia ndani ya bank kwa ajili ya shughuli za bank anazozijua yeye.

Askari hao walimfuata tena ndani na kumwambia akatoe gari lakini mwanamke huyo kwa nyodo alimjibu askari huyo aachane nae.

Kuona hivyo askari walikwenda kutoa upepo kwenye matairi ya gari yake ili kama alikuwa na watu wengine wenye nia mbaya wahindwe kutekeleza mpango wao.

Yule mwanamke aliporudi na kukuta gari yake imetokewa upepo alliukiza watu na kuambiwa ni askari waliotoa upepo. Basi alikwenda moja kwa moja kwenye gari na kutoa bastola kisha akaenda kwa askari polisi waliopo huku akiwatisha atawaua. Katika hali ya taharuki yule mwanamke akakoki bunduki kwa lengo la kuitumia na ndipo askari akipomuhai risasi ya mkononi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio mwanamke huyo hajulikani alipata wapi ujasiri wa aliyoyafanya.

Mbinu inayotumiwa na Matajiri wa Urusi kukwepa foleni

6

7

8

2

3
Sote tunafahamu kwamba Ambulance ni magari yanayotumika kubeba na kuwaisha wagonjwa kutoka sehemu fulani kwenda sehemu nyingine na uwapo barabarani kama dereva ni lazima upishe Ambulance inayopita ili iokoe maisha ya mgonjwa ila matumizi ya Ambulance huko Urusi sio ya Wagonjwa peke yake.

Unaambiwa moja ya tabia za matajiri wa Urusi ni kukodi magari feki ya wagonjwa (Ambulance) ili kukwepa foleni hasa kwenye jiji la Moscow ambalo lipo kwenye list ya majiji yenye foleni kubwa  sana duniani ambapo matajiri hao hulipia safari moja kwa zaidi ya shilingi laki tatu za kibongo.

Ambulance hizi feki zinatofautiana na zile za hospitali kwa ndani lakini kwa nje ni kama Ambulance ya kweli ambapo hizi feki ndani yake kunapatikana huduma kama za TV, vinywaji vya aina mbalimbali, hata makochi yametengenezwa vizuri sana ambapo uzuri huo unafananishwa na magari ya kifahari ya Limousine na wakati mwingine kwenye hizi ambulance kunakua na Wanawake maalum ndani yake kwa ajili ya kutoa kampan kwa mteja.

Rais Putin na Waziri wake mkuu huwa wanapita na msafara huku magari yao yakiwa yana taa maalum za blue ambazo ni ishara kwa kila mmoja kwamba msafara wa kiongozi mkuu uko barabarani.

Polisi wamekua wakijaribu kuzisimamisha lakini sio zoezi ambalo lina mafanikio.

Taarifa ya polisi na picha 7 za watuhumiwa waliokamatwa na kiganja cha mkono wa Binadamu Mwanza. (Onyo: picha zinatisha )

6

WAGANGA wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja wamenaswa jijini Mwanza wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoaminika kuwa wa binaadamu ambapo walikamatwa kwenye eneo la ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na kufanikiwa kuwakamata.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph Konyo amethibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
 
Konyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
 
Taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo mteja angehitaji.
2

kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni baada ya kuonyesha kiungo hicho.
5

3

4

1

7

Baadhi ya picha za Ajali ya Treni iliyoua Nairobi Kenya leo asubuhi

AJALI MBAYA YATOKEA KENYA YAHUSISHA TRENI NA BUS LA ABIRIA2
Treni Nairobi1

Watu 11 wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja viungani mwa mji wa Nairobi.
 


Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu 34 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini, Kwa mujibu wa shirika la Red Cross, idadi ya majeruhi imefika 34 na wamepelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.
Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kuwa katika hali mbaya.
 
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa kwa upande.
 
Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.
 
Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.
 
Ajali hiyo imetokea asubuhi wakati wa msongamano wa watu na magari huku watu wengi wakiwa katika haraka kuu kuelekea kazini