Unaambiwa moja ya tabia za matajiri wa Urusi ni kukodi magari feki ya wagonjwa (Ambulance) ili kukwepa foleni hasa kwenye jiji la Moscow ambalo lipo kwenye list ya majiji yenye foleni kubwa sana duniani ambapo matajiri hao hulipia safari moja kwa zaidi ya shilingi laki tatu za kibongo.
Ambulance hizi feki zinatofautiana na zile za hospitali kwa ndani lakini kwa nje ni kama Ambulance ya kweli ambapo hizi feki ndani yake kunapatikana huduma kama za TV, vinywaji vya aina mbalimbali, hata makochi yametengenezwa vizuri sana ambapo uzuri huo unafananishwa na magari ya kifahari ya Limousine na wakati mwingine kwenye hizi ambulance kunakua na Wanawake maalum ndani yake kwa ajili ya kutoa kampan kwa mteja.
Rais Putin na Waziri wake mkuu huwa wanapita na msafara huku magari yao yakiwa yana taa maalum za blue ambazo ni ishara kwa kila mmoja kwamba msafara wa kiongozi mkuu uko barabarani.
Polisi wamekua wakijaribu kuzisimamisha lakini sio zoezi ambalo lina mafanikio.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.