Sunday, 13 October 2013

UFO SARO AFANYIWA UPASUAJI!!


Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mtu aliyedaiwa ni mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua.
Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.

ANGALIA VIDEO MPYA TOKA KWA LUCCI-SUMU

Nimeridhishwa na ubora wa video na nyimbo yenyewe big up director Nisher na Lucci .

Like page yetu ya facebook kisha toa comment yako kuhusu nyimbo hii

RAIS KENYATA KUTOHUDHURIA KESI MAHAKAMA YA THE HEGI

Uhuru Kenyatta 11

Imefahamika kwamba Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hatohudhuria vikao vya kesi dhidi yake kwenye Mahakama ya ICC The Hague haya yakiwa ni maafikiano ya viongozi wa Afrika kwenye kongamano la Umoja wa Afrika Ethiopia.

Mkutano huo unakusudia kuwatuma Marais watano wa Afrika nchini Uholanzi ili kuitaka Mahakama hiyo kuahirisha kesi ya rais Kenyatta itakayoanza November 12 ambapo pia mkutano huu umesema hata Naibu Rais William Ruto hafai kushtakiwa kwenye Mahakama hiyo ya ICC.

KESHO NI NYERERE DAY HEBU ANGALIA NA FAHAMU MACHACHE TOKA KATIKA MAKUMBUSHO YA MWALIMU JULIUS. K.NYERERE

Hili ni jumba la Makumbusho ya Mwalimu J.K.Nyerere, Butiama mkoani Mara. Ushawahi kutembelea hapa?


Mchezo wa Bao huchezwa na makabila mengi hapanchini Mwalimu J.K Nyerere amekuwa akicheza na kuupenda mchezo huo hata baadhi ya vyama miaka ya sasa kumuenzi kwa kufanya mashindano mbalimbali nchini. Bao hili alipewa na wananchi wa Ndanda.

Joho la Uhitimu.

Hivi ni baadhi ya viatu alivyokuwa akivaa Hayati Mwalimu J.K.Nyerere. Mwalimu alipenda zaidi viatu vya kutumbukiza, pembeni kama mkoba ni redio yake. Itizame kwa uzuri katika picha inayofuata.


Ni Redio aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kusikiliza habari mbalimbali alipenda pia kuitumia katika baadhi ya ziara zake za ndani na nje ya nchi. Redio hii alipewa zawadi huko Ujerumani mwaka 1969.

A gift of traditional stool given to Mwl. Nyerere by the residents of Dar-es-Salaam after the victory of Kagera war in 1978 - 1979.

Jiwe la kusagia nafaka huitwa 'Ombwe' na dogo huitwa Esyo, kwa kawaida kazi ya kusaga hufanywa na wanawake. Chakula kikuu cha wazanaki ni ugali, huliwa kwa nyama, samaki na mboga za majani.

Picha nazo zipo

Urithi wa asili wa Tamaduni za kizanaki silaha za jadi, vifaa vya nyumbani, ala za muziki, mapambo ya asili, lugha, mila, desturi - nk. Vyte utavikuta kwenye nyumba hii ya makumbusho ya Mwalimu.

DIAMOND HANA PAPARA NA MTU!!


HONGERA TEMBA KWA KUPATA MTOTO WA KIUME!!!

tmb
Kutoka TMK, msanii ambaye aliwahi kuwa mchezaji basketball hadi kupewa nafasi ya kujiunga na jeshi kutokana na kucheza mchezo huo lakini ilishindikana kutokana na kuwa na tatoo. Habari nzuri ni kwamba Temba amepata mtoto mwingine na kufanya idadi ya watoto wake kuwa wawili. Mtoto huyo wa kiume amepewa jina laMelyvin ambaye pia dada yake anaitwa Mishell
2
Mtoto Melyvin
1
Mishell Temba

RAIS KIKWETE AONDOKA ADDIS ABABA BAADA YA KUHUDHURIA KIKAO CHA SIKU MOJA CHA VIONGOzI WA UMOJA WA AFRIKA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Waziri wa Sheria na Katika Mhe. Mathias Chikawe na Balozo wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz baada ya kuhudhuria kikao cha siku moja cha viongozi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa Oktoba 12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia Bw. Nsavike Ndatta baada ya kuhudhuria kikao cha siku moja cha viongozi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa Oktoba 12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Waziri wa Sheria na Katika Mhe. Mathias Chikawe na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz baada ya kuhudhuria kikao cha siku moja cha viongozi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa Oktoba 12.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole baada ya viongozi hao kuhudhuria kikao cha siku moja cha viongozi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia Oktoba 12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole baada ya viongozi hao kuhudhuria kikao cha siku moja cha viongozi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia Oktoba 12.

MWANDISHI WA HABARI WA ITV NA RADIO ONE UFO SARO APIGWA RISASI NA ANAYEDAIWA KUWA MCHUMBA WAKE

 
Mtangazaji wa ITV, Ufo Saro (pichani) amepigwa risasi na kijana Mushi anayeripotiwa kuwa ni mume au mchumba wa mtangazaji huyo, kwa mujibu wa taarifa za awali mama mzazi wa Ufoo amepigwa risasi ya kifuani na kufa papo hapo leo alfajiri.

Mushi amempiga risasi ya tumbo na mguuni Ufo ambaye alikuwa anaendelea na matibabu Hospitali ya Tumbi Kibaha na tukio hili limetokea Kimara. Baada ya tukio hilo, Mushi alijipiga risasi na kufa papo hapo. SOURCE RADIO ONE

Habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Ufuo amekimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu zaidi.