Manispaa ya Bukoba haitoshi tena mara baada ya
wanamuziki kuwa na hamu ya kufunika na kuonesha kuwa wanaweza kuonesha uwezo
wao na kuwapagawisha wapenda burudani wote waliopo mjini humu… kupitia show
kali ya Vision Music Ambassador (VMA) inayoandaliwa na Redio Vision Fm
(100.0MHz)
Haya yanatokea ikiwa zimebaki siku chache kwa Vision
Fm radio iliyopo Kibeta,Bukoba Tanzania kuandaa jukwaa la kuinua vipaji vya
wasanii wa mji wa bukoba pamoja na kagera kwa ujumla ili kuwapa vijana nafasi
mpya ya ajira ambayo kwa sasa muziki umewaajiri vijana wengi hapa nchini
Tanzania.
Mratibu wa maonyesho hayo Bw. Valerian Rugalabamu
amesema kwa upande wa redio ambao ndio waandaaji wakuu wa show hii wamejipanga vizuri kuwaonesha wakazi wa
bukoba wapenda burudani na maendeleo kwa ujumla kwamba kila jambo linawezekana
na kwamba Vision fm redio inathamini vipaji vya vijana wa mkoa wa kagera ambao
ndio walengwa hasa.