Friday, 6 September 2013

MSANII SAIDA KALORI AWASILI BUKOBA KWA AJILI YA SHOW JUMAMOSI HII USIKU.



Baada ya kuzushiwa kuwa amefariki msanii SAIDA Kalori sasa ameamua kurudi nyumbani na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa yupo hai na anaendelea kukonga nyoyo za mashabiki wake.


Saida anatarajia kufanya show babkubwa usiku wa Jumamosi hii mjini BUKOBA,akisindikizwa na wasanii wa VISION MUSIC AMBASSADOR(VMA) akiwemo Yombo Man,Kamdingi Fulani, Bk Sande,Shemela,White chapombe,Dogo Wisdom,Kingdata, Young zilla, Babu Rweyemamu, T.kasha, Enock, Luv B, Fireborn, Mr. M, Fred na wengine kibao toka VMA.


Wasanii wengine watakaompa shavu Saida ni pamoja na Kajei Poda toka Nairobi Kenya, Papaa Kishaju, Sadath Ngemela n.k


Mcheki Saida na Kajei Poda wakifanya mahojiano redio vision fm kuhusu show ya kesho mjini Bukoba 


Saida Kalori, Kajei poda na mkurugenzi Tivol Bw. Madaraka.




                                Msanii Saida Kalori



Mtangazaji Matrida Leopord akiendelea na mahojiano na msanii Saida Kalori,Kajei poda pamoja na Bw. Madaraka.