Mtangazaji na Produzer wa Vision fm radio 100.0MHz, Michael
Bwoma A.K.A De Marco akiwafanyia interview wasanii ambao tayari wamekubari na
kuthibitisha ushiriki wao kwenye show kali ya VISION MUSIC AMBASSADOR (VMA) itakayofanyika jumapili ya
tarehe 19,05,2013 katika ukumbi wa
Bukoba Club.
Wasanii hawa walifika katika studio za Vision fm
radio kuitikia wito wa Tangazo la kuwaita wasanii wachanga na wakongwe ili
walete Cds zao na kupata nafasi ya kuwa washiriki na hadi kufikia leo jumamosi
ni zaidi ya wanamuziki hamsini wamejitokeza kuweza kujihakikishia nafasi ya
kufanya matumbuizo ya VMA kila siku ya jumapili ya mwisho wa mwezi.
Wasanii hawa
wameonekana kuwa wenye hari na kwamba wapo tayari kwaajili ya kufunika katika
jukwaa la VISION MUSIC AMBASSADOR…
Tafadhari usikose kufika siku hiyo kwani kuna mambo
mengi yameandaliwa kwaajili yako na kwamba kutakuwa na uzinduzi rasmi wa
kipindi cha THE BASH mara baada ya kuwa kimepikwa upya na kuwa show ambayo
itaongoza hapa Mjini Bukoba na Kagera kwa ujumla..