Sunday, 13 October 2013

MWANDISHI WA HABARI WA ITV NA RADIO ONE UFO SARO APIGWA RISASI NA ANAYEDAIWA KUWA MCHUMBA WAKE

 
Mtangazaji wa ITV, Ufo Saro (pichani) amepigwa risasi na kijana Mushi anayeripotiwa kuwa ni mume au mchumba wa mtangazaji huyo, kwa mujibu wa taarifa za awali mama mzazi wa Ufoo amepigwa risasi ya kifuani na kufa papo hapo leo alfajiri.

Mushi amempiga risasi ya tumbo na mguuni Ufo ambaye alikuwa anaendelea na matibabu Hospitali ya Tumbi Kibaha na tukio hili limetokea Kimara. Baada ya tukio hilo, Mushi alijipiga risasi na kufa papo hapo. SOURCE RADIO ONE

Habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Ufuo amekimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.