Wakati baadhi
ya wanasiasa wakiwa na mawazo ya kuachana na siasa baadhi yao wakidai inapoteza
muda , hii imekuwa kinyume kwa msanii Shemela maarufu kama Shemela daima toka Kiziba Misenyi baada ya hivi punde kutangaza
rasmi kuwa anaacha muziki na kuingia katika siasa.
Shemela
anayetamba katika vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini na nyimbo mpya
iitwayo malipo ni kesho,amesema ameamua kuingia katika siasa baada ya kuona
baadhi ya wanasiasa wanaleta longo longo kibao hasa kijijini kwao Kiziba.
Pamoja na
kuacha game la muziki Shemela anasema anajivunia mafanikio yake aliyopata mpaka
sasa,ikiwa ni pamoja na heshima aliyonayo kwa jamii kutokana na kazi yake ya muziki,pia
kupitia nyimbo yake ya kitambo kidogo iitwao Amenibamba amepata gari lake na
sasa ana kiwanja ambapo ameanza kujenga nyumba yake.
Aidha
shemela amewashauri wasanii wenzake kuwa, heshima na uvumilivu ni nguzo kuu
katika mafanikio hivyo wasanii wakifuata hayo watafika mbali.
Shemela ni
miongoni mwa wasanii waliopo ndani ya VISION MUSIC AMBASSADOR na Jumamosi hii
Septemba 14,atafanya tamasha Bunazi
Misenyi ikiwa ni show yake ya mwisho na atawaaga rasmi mashabiki wake wa
Misenyi.
Hizi ni baadhi
ya picha wakati nikifanya interview ya tv show ya chanel 12 Misenyi na msanii
Shemela
|