WAGANGA
wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja wamenaswa jijini Mwanza wakiwa na
kiungo cha mkono wa kulia unaoaminika kuwa wa binaadamu ambapo walikamatwa
kwenye eneo la ziwani na
Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi
kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na
kufanikiwa kuwakamata.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph
Konyo amethibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi
ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye
karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
Konyo ambaye pia ni
Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa
watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga
wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Taarifa zilizotolewa
katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo
kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa
wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo
mteja angehitaji.
kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni baada ya kuonyesha kiungo hicho.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.