Wednesday, 2 October 2013

USHASIKIA HII!!!



TANGAZO
VISION MUSIC AMBASSADOR JUMAPILI HII OKTOBA 6 INAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA MATUMIZI NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA,


KAMPENI HII ITAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA MKOA KAGERA KANALI  MSTAAFU  FABIANI  MASAWE KATIKA UKUMBI WA BUKOBA CLUB KUANZIA SAA 3 ASUBUHI,


UZINDUZI HUU UTAHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI, KISIASA, DINI, WAFANYABISHARA,TAASISI MBALIMBALI, WANAVYUO NA WATU WOTE KWA UJUMLA,
KIINGILIO: 5000 WAKUBWA
                       3000 WADOGO 


KWA ULIYEMBALI AMBAYE UNAUNGA MKONO KAMPENI HII ITAKAYOFANYIKA  KWA MKOA MZIMA WA KAGERA KWA KIPINDI CHA MIEZI SITA,

ILI TUFANIKISHE KAMPENI HII NA KUWAOKOA WANAOATHIRIKA UNAWEZA KUCHANGIA MCHANGO WAKO KWA NJIA YA M-PESA KATIKA NAMBA 0755 001051 AU KATIKA  AKAUNTI YA BENKI NMB, AKAUNTI NAMBA NI 318 660 03 60 JINA LA AKAUNTI NI RADIO VISION FM 



MMOJA  WETU AKIATHIRIKA WOTE TUMEATHIRIKA
KARIBUNI SANA!!!

KAMPENI YA KUPINGA MATUMIZI NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA INAYOENDESHWA NA VISION MUSIC AMBASSADOR,JUMAPILI HII OKTOBA 6 ITAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA MKOA KAGERA KANALI MSTAAFU FABIANI MASAWE.......


Mkuu wa mkoa Kagera kanali mstaafu Fabian Masawe,ameunga mkono kwa asilimia mia moja kampeni hii ya kupinga matumizi na biashara ya madawa ya kulevya na kutoa wito kwa watanzania kuunga mkono kampeni hii kwani kwa sasa taifa letu limegubikwa na aibu kubwa ya madawa haya,ikiwa ni pamoja na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Kamanda wa zimamoto mkoa wa Kagera Inspecta Salumu Mohamed Omary,atoa wito kwa serikali kuongeza nguvu ya kupambana na uingiaji wa madawa ya kulevya,ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kudhibiti njia za maji na viwanja vya ndege kwani madawa hayawezi kutumika endapo hayaingii.
Assistance Inspector Jeshi la magereza mkoa wa Kagera Inspecta John Masalu,akieleza namna madawa ya kulevya yanavyoleta athari kwa watumiaji,wauzaji,wasambazaji hata taifa kwa ujumla.

Vijana wa kimasai wao wanasema Ugoro ni moja kati ya madawa ya kulevya na ni hatari sana kwa afya yako.