Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu
34 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini, Kwa mujibu wa shirika
la Red Cross, idadi ya majeruhi imefika 34 na wamepelekwa katika hospitali kuu
ya Kenyatta.
Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana
kuwa katika hali mbaya.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema
kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa kwa upande.
Inaarifiwa watu sita walifariki papo
hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.
Wengine wengi wamejeruhiwa kwa
mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.
Ajali hiyo imetokea asubuhi wakati
wa msongamano wa watu na magari huku watu wengi wakiwa katika haraka kuu
kuelekea kazini
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.