Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri
wake wa usalama Joseph Ole Lenku imesema kuwa watu 59 wamefariki katika
shambulizi la kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175
kujeruhiwa.
Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi
ya magaidi walio ndani ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano na
haijulikani ikiwa wanawazulia waathiriwa au waathiriwa wamejificha katika sehemu
mbali mbali za jumba la Westgate.
Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao
wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.
Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya
waliofariki ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa
Canada na raia wawili wa Ufaransa.
Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima
wakabiliwe na mkono wa sheria.
Jamaa na marafiki waliofika kujua
hali ya jamaa zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa
walifariki kutokana na majeraha yao.
Baadhi ya wananchi wakikimbia wakati mashambulizi yakiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.