Duka la kifahari lililoshambuliwa la
Westgate katika mtaa wa Westlands Nairobi.
Al shabaab: ''Kenya ilipuuza onyo letu''
Afisaa mmoja mkuu wa kundi la
kigaidi la Alshabaab, amesema kuwa kundi hilo ndilo limehusika na
shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westgate mjini Nairobi Kenya.
Kwa mujibu wa Afisaa huyo
mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita
vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.
Wanajeshi wa Kenya wamekuwa nchini
humo tangu mwaka 2011 kama sehemu ya juhudi za muungano wa Afrika kutaka
kurejesha uthabiti nchini Somalia.
Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya
zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.
Baadhi ya watu waliofanikiwa
kukimbilia usalama wao
Wanamgambo wa Al Shabaab kupitia kwa
mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo
walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake nchini humo
kupambana dhidi yao.
Kundi hilo limesema limekuwa likitoa
onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia,
athari zitakuwa mbaya mno.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al
Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua
waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
Taarifa hiyo ya Twitter ilisema kuwa
Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba
wasomali nchini Somalia.
Taharuki ilianza hii jana saa saba
mchana wakati watu wanaokisiwa kuwa kumi walipovamia jengo la kifahari la
Westgate na kuwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli
zao za kawaida.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.