Saturday, 7 December 2013

KIGOMA ALL STARS NDANI Y A LEKADUTIGITE EAST AFRICAN AND DRC CONGO FOR PEACE TOUR MJINI MOMBASA KENYA

DSC_0085 
Hawa ni wasanii kutoka Kigoma All Stars wakiwa katika show ya pamoja Mombasa Kenya,katika moja kati ya tour ya Kigoma All stars waliyoipa jina la Lekadutigite East African and Drc Congo for Peace Tour.
DSC_0007
Wasanii ambao watakuepo ni pamoja na Abdul Kiba,Mwasiti,Recho,Queen Darlin,Maunda zoro,Chegge,Ommy Dimpoz,Diamond Platnumz na wasanii wengine.
DSC_0086
Show hii inafanyika pemben mwa fukwe za bahari ya hindi Sehemu inaitwa Big Tree Beach.
DSC_0090                      Jukwaa likiwa katika matengenezo kwa ajili ya show
DSC_0011

Use Facebook to Comment on this Post

Friday, 1 November 2013

SERIKALI YASITISHA OPARESHENI TOKOMEZA

SERIKALO YAAMUA KUSITISHA OPERESHENI TOKEMEZA 



Serikali imeamua kusitisha Oparesheni TOKOMEZA ili kupisha uchunguzi Kwa kuzingatia uzito wa hoja zilizotolewa na Mbunge wa Sikonge, SAID NKUMBA na ile ya Mbunge wa Mwibala KANGI LUGOLA kuhusiana na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu pembezoni mwa hifadhi za taifa,.

Akitoa taarifa ya awali Bungeni yenye lengo la kudhibiti tatizo la ujangili wa tembo na wanyama wengine Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi HAMIS KAGASHEKI, ameagiza kuachiwa kwa mifugo .
 
Akiufunga mjadala huo, Spika wa Bunge ANNE MAKINDA amesema kuhusiana na Oparesheni TOKOMEZA, bunge linaiachia Kamati ya Maliasili na Utalii kulipatia ufumbuzi huku lile la migogoro ya ardhi itaundiwa Kamati teule itakayofanya tathmini na kutoa maamuzi.
 
Zaidi ya Ng’ombe 4,000 wanaoshikiliwa na Serikali katika maeneo
mbalimbali nchini walitarajiwa kupigwa mnada kinyume na taratibu ili kushinikiza wafugaji kutoa rushwa kwa watendaji wanaoendesha Oparesheni TOKOMEZA ili mifugo yao iachiwe.
Toa Maoni Yako

Video hii imetazamwa zaidi ya mara milioni 15

mtoto
Kutokana na udogo wa huyu mtoto na jinsi hisia zinavyomteka mpaka kuanza kutoa machozi kutokana na mama yake kuimba nyimbo ndio kilichofanya kila mmoja akimbilie kuitazama video hii na kufikia kutazamwa zaidi ya mara milioni 15 na laki 8 toka imewekwa October 18 2013

Thursday, 31 October 2013

forbesMtandao maarufu kwa kutoa list mbalimbali ikiwemo ya watu matajiri duniani, wakati huu wametoa list ya watu wenye nguvu sana duniani. Mwaka jana namba moja alikuwa rais wa taifa kubwa dunia Barrack Obama. Mwaka huu mambo yamekuwa tofauti kwa kumuona bwana Obama akishuka kutoka kwenye hiyo nafasi yake.



Watu wengine maarufu waliopo kwenye top five ni  Xi Jinping mwenyekiti wa chama cha kikomunisti cha China,Pope Francis,Angela Merkel kutoka Ujerumani na Vladimir Putin kutoka Russia ambaye ndiyo namba moja akifuatiwa na Barack Obama namba mbili.
Untitled

 

Walemavu
Citizen TV Kenya wanaripoti kwamba huko Mombasa wamekamatwa watu 26 wenye ulemavu ambao walichukuliwa kutoka Tanzania na Mwanamke Mtanzania ili kwenda kufanya biashara ya kuomba pesa na baadae jioni Mwanamke huyo anapitia mahesabu huku akiwa amewaweka walemavu hawa kuishi kwenye nyumba moja huko Mwembe tayari.
Mwanamke huyu nadaiwa kuwa na mtindo wa kuagiza Walemavu kuchukuliwa Tanzania na kuingizwa Kenya kupitia Taveta na Lungalunga ambapo anawatumia kibiashara yeye na washirika wake ambapo mpaka sasa washukiwa saba wametiwa mbaroni kutokana na hii ishu.
Taarifa inasema ombaomba hawa ambao wanatoka Shinyanga, Mwanza, Musoma na Bukoba wakiwa mitaani kuomba, wakipata shilingi mia tano ya Kenya tajiri anachukua shilingi 300 na anamuachia shilingi 200.
Mmoja wa Walemavu hao anasema ‘kabla ya kuletwa Kenya tunapewa ahadi nzuri za kuvutia kwenda, mimi niliahidiwa kupewa Baiskeli lakini kinachotokea sasa hivi ni kwamba nikipata hiyo pesa ya kuombaomba, Mwanamke huyu ndio anapanga bajeti zake wala hamna anachofanya’

Wednesday, 30 October 2013

BREAKING NEWS: MWANAMKE MMOJA APIGWA RISASI TRA JIJINI ARUSHA

Mwanamke mmoja amepigwa risasi ya mkononi kutokana na uzembe wake mwenyewe.

Mwanamke huyo alifika maeneo ya TRA ambako kuna tawi la CRDB - Mapato na kupaki gari eneo lisiloruhusiwa. Askari walimuelekeza eneo hilo haliruhusi kupaki gari lakini alikataa na kuingia ndani ya bank kwa ajili ya shughuli za bank anazozijua yeye.

Askari hao walimfuata tena ndani na kumwambia akatoe gari lakini mwanamke huyo kwa nyodo alimjibu askari huyo aachane nae.

Kuona hivyo askari walikwenda kutoa upepo kwenye matairi ya gari yake ili kama alikuwa na watu wengine wenye nia mbaya wahindwe kutekeleza mpango wao.

Yule mwanamke aliporudi na kukuta gari yake imetokewa upepo alliukiza watu na kuambiwa ni askari waliotoa upepo. Basi alikwenda moja kwa moja kwenye gari na kutoa bastola kisha akaenda kwa askari polisi waliopo huku akiwatisha atawaua. Katika hali ya taharuki yule mwanamke akakoki bunduki kwa lengo la kuitumia na ndipo askari akipomuhai risasi ya mkononi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio mwanamke huyo hajulikani alipata wapi ujasiri wa aliyoyafanya.

Mbinu inayotumiwa na Matajiri wa Urusi kukwepa foleni

6

7

8

2

3
Sote tunafahamu kwamba Ambulance ni magari yanayotumika kubeba na kuwaisha wagonjwa kutoka sehemu fulani kwenda sehemu nyingine na uwapo barabarani kama dereva ni lazima upishe Ambulance inayopita ili iokoe maisha ya mgonjwa ila matumizi ya Ambulance huko Urusi sio ya Wagonjwa peke yake.

Unaambiwa moja ya tabia za matajiri wa Urusi ni kukodi magari feki ya wagonjwa (Ambulance) ili kukwepa foleni hasa kwenye jiji la Moscow ambalo lipo kwenye list ya majiji yenye foleni kubwa  sana duniani ambapo matajiri hao hulipia safari moja kwa zaidi ya shilingi laki tatu za kibongo.

Ambulance hizi feki zinatofautiana na zile za hospitali kwa ndani lakini kwa nje ni kama Ambulance ya kweli ambapo hizi feki ndani yake kunapatikana huduma kama za TV, vinywaji vya aina mbalimbali, hata makochi yametengenezwa vizuri sana ambapo uzuri huo unafananishwa na magari ya kifahari ya Limousine na wakati mwingine kwenye hizi ambulance kunakua na Wanawake maalum ndani yake kwa ajili ya kutoa kampan kwa mteja.

Rais Putin na Waziri wake mkuu huwa wanapita na msafara huku magari yao yakiwa yana taa maalum za blue ambazo ni ishara kwa kila mmoja kwamba msafara wa kiongozi mkuu uko barabarani.

Polisi wamekua wakijaribu kuzisimamisha lakini sio zoezi ambalo lina mafanikio.

Taarifa ya polisi na picha 7 za watuhumiwa waliokamatwa na kiganja cha mkono wa Binadamu Mwanza. (Onyo: picha zinatisha )

6

WAGANGA wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja wamenaswa jijini Mwanza wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoaminika kuwa wa binaadamu ambapo walikamatwa kwenye eneo la ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na kufanikiwa kuwakamata.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph Konyo amethibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
 
Konyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
 
Taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo mteja angehitaji.
2

kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni baada ya kuonyesha kiungo hicho.
5

3

4

1

7