Friday, 1 November 2013

SERIKALI YASITISHA OPARESHENI TOKOMEZA

SERIKALO YAAMUA KUSITISHA OPERESHENI TOKEMEZA 



Serikali imeamua kusitisha Oparesheni TOKOMEZA ili kupisha uchunguzi Kwa kuzingatia uzito wa hoja zilizotolewa na Mbunge wa Sikonge, SAID NKUMBA na ile ya Mbunge wa Mwibala KANGI LUGOLA kuhusiana na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu pembezoni mwa hifadhi za taifa,.

Akitoa taarifa ya awali Bungeni yenye lengo la kudhibiti tatizo la ujangili wa tembo na wanyama wengine Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi HAMIS KAGASHEKI, ameagiza kuachiwa kwa mifugo .
 
Akiufunga mjadala huo, Spika wa Bunge ANNE MAKINDA amesema kuhusiana na Oparesheni TOKOMEZA, bunge linaiachia Kamati ya Maliasili na Utalii kulipatia ufumbuzi huku lile la migogoro ya ardhi itaundiwa Kamati teule itakayofanya tathmini na kutoa maamuzi.
 
Zaidi ya Ng’ombe 4,000 wanaoshikiliwa na Serikali katika maeneo
mbalimbali nchini walitarajiwa kupigwa mnada kinyume na taratibu ili kushinikiza wafugaji kutoa rushwa kwa watendaji wanaoendesha Oparesheni TOKOMEZA ili mifugo yao iachiwe.
Toa Maoni Yako

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.