Wednesday, 2 October 2013

KAMPENI YA KUPINGA MATUMIZI NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA INAYOENDESHWA NA VISION MUSIC AMBASSADOR,JUMAPILI HII OKTOBA 6 ITAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA MKOA KAGERA KANALI MSTAAFU FABIANI MASAWE.......


Mkuu wa mkoa Kagera kanali mstaafu Fabian Masawe,ameunga mkono kwa asilimia mia moja kampeni hii ya kupinga matumizi na biashara ya madawa ya kulevya na kutoa wito kwa watanzania kuunga mkono kampeni hii kwani kwa sasa taifa letu limegubikwa na aibu kubwa ya madawa haya,ikiwa ni pamoja na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Kamanda wa zimamoto mkoa wa Kagera Inspecta Salumu Mohamed Omary,atoa wito kwa serikali kuongeza nguvu ya kupambana na uingiaji wa madawa ya kulevya,ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kudhibiti njia za maji na viwanja vya ndege kwani madawa hayawezi kutumika endapo hayaingii.
Assistance Inspector Jeshi la magereza mkoa wa Kagera Inspecta John Masalu,akieleza namna madawa ya kulevya yanavyoleta athari kwa watumiaji,wauzaji,wasambazaji hata taifa kwa ujumla.

Vijana wa kimasai wao wanasema Ugoro ni moja kati ya madawa ya kulevya na ni hatari sana kwa afya yako.



No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.