Saturday, 4 May 2013

WAKALI WA MIDUNDO MBALI MBALI MKOANI KAGERA WATAMBIANA KUFUNIKANA VMA








Mtangazaji na Produzer wa Vision fm radio 100.0MHz, Michael Bwoma A.K.A De Marco akiwafanyia interview wasanii ambao tayari wamekubari na kuthibitisha ushiriki wao kwenye show kali ya VISION MUSIC AMBASSADOR (VMA) itakayofanyika jumapili ya tarehe 19,05,2013 katika ukumbi wa Bukoba Club.

Wasanii hawa walifika katika studio za Vision fm radio kuitikia wito wa Tangazo la kuwaita wasanii wachanga na wakongwe ili walete Cds zao na kupata nafasi ya kuwa washiriki na hadi kufikia leo jumamosi ni zaidi ya wanamuziki hamsini wamejitokeza kuweza kujihakikishia nafasi ya kufanya matumbuizo ya VMA kila siku ya jumapili ya mwisho wa mwezi. 

Wasanii hawa wameonekana kuwa wenye hari na kwamba wapo tayari kwaajili ya kufunika katika jukwaa la VISION MUSIC AMBASSADOR… 

Tafadhari usikose kufika siku hiyo kwani kuna mambo mengi yameandaliwa kwaajili yako na kwamba kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kipindi cha THE BASH mara baada ya kuwa kimepikwa upya na kuwa show ambayo itaongoza hapa Mjini Bukoba na Kagera  kwa ujumla..

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.