Thursday, 2 May 2013

HOMA YA JIJI VISION MUSIC AMBASSADOR YA 100.0MHz




Manispaa ya Bukoba haitoshi tena mara baada ya wanamuziki kuwa na hamu ya kufunika na kuonesha kuwa wanaweza kuonesha uwezo wao na kuwapagawisha wapenda burudani wote waliopo mjini humu… kupitia show kali ya Vision Music Ambassador  (VMA) inayoandaliwa na Redio Vision Fm (100.0MHz)
Haya yanatokea ikiwa zimebaki siku chache kwa Vision Fm radio iliyopo Kibeta,Bukoba Tanzania kuandaa jukwaa la kuinua vipaji vya wasanii wa mji wa bukoba pamoja na kagera kwa ujumla ili kuwapa vijana nafasi mpya ya ajira ambayo kwa sasa muziki umewaajiri vijana wengi hapa nchini Tanzania.
Mratibu wa maonyesho hayo Bw. Valerian Rugalabamu amesema kwa upande wa redio ambao ndio waandaaji wakuu wa show  hii wamejipanga vizuri kuwaonesha wakazi wa bukoba wapenda burudani na maendeleo kwa ujumla kwamba kila jambo linawezekana na kwamba Vision fm redio inathamini vipaji vya vijana wa mkoa wa kagera ambao ndio walengwa hasa.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.