Monday, 20 May 2013

UZINDUZI WA VISION MUSIC AMBASSADOR WANYIMA WATU USINGIZI KAGERA!!!!!!

VISION MUSIC AMBASSADOR inayodhaminiwa na redio vision fm iliyopo BUKOBA,hatmaye imezinduliwa rasmi MEI 19,2013 katika ukumbi wa BUKOBA CLUB mjini BUKOBA,huku kila msanii akionyesha makeke yake kwa stage,wakazi wa KAGERA nao hawakuwa nyuma kwani walitoka kila kona ya mkoa wa KAGERA kuja kutoa sapoti kwa UP COMING ARTIST na RISING STAR wa KAGERA,check baadhi ya picha...


                                         
 Mshiriki toka MULEBA SHADIAPHIY YASSIN a.k.a  SHARAYAITI akiwa na kundi lake wakiwapa burudani mafans wa VISION MUSIC AMBASSADOR  katika ukumbi wa BUKOBA CLUB...
 FILEMON OBED a.k.a FIRE MAN naye hakuwa nyuma,hapa anakonga nyoyo 

 Mshiriki wa VMA toka manispaa ya BUKOBA akiwakilisha pande ya KASHAI,DENIC THOMAS a.k.a SIzO MAN akiwa kwa stage la VMA, yaani ACHAAAA KABISAAAAAAAAAAAAAAAA!!!
 Dogo wa kidato cha kwanza toka BUKOBA SEKONDARI akichana mistari katika track yake NESTORY YOEL a.k.a WILL WISHER pamoja na AHMED PAUL a.k.a PING PO!! toka SAUTI UNIVERSITY palikuwa hapotoshi!!!
Hapa tena wakiendelea na mashambulizi dogo akizidi kuchana mistari,PING PO na kwa nyuma katikati ni WILL WISHER, weeeeeeeeee!!! kaa mbaaaaaliii,moto wa VMA ni balaaaaaaaaaaaaa!!!!
MR MOSSI ndani ya VMA akiwapa raha mashabiki wake kwa track mbalimbali ikiwemo AMALILA!!! duuuh!!!Safiiiiiiiiiiiii
Mshikaji anawakilisha MULEBA,anaitwa YOMBO MAN mzee wa MAWIO na MACHWEO,ilikuwa ni noooomaaaaa,maana viuno vilihusika pale kati yaani ni balaaaaaaaaaaa!!
MR CHINGA anayefanya vyema katika nyimbo yake ya WIPOLO katika picha wa kwanza kushoto akipewa kampani na Rastafarian wa kwanza kulia,KHEEEEEEEEEEEE!!!!!! MR CHINGA si akapanda na nyoka aiseeeee!! duuh!!!!! mcheki kabebwa na jamaa hapo katikati,usiombeeeeee!!
MR CHINGA anaendelea kuwapa raha mashabiki wa VMA ndani ya ukumbi wa Bk. CLUB

Zamu ya BABU RWEYEMAMU mshindi wa miaka 50 ya uhuru,shindano lililoandaliwa na VISION FM nayo ikafika, BABU RWEYEMAMU akajiachia kiasili!!!!! Yaaaani ilikuwa rahaaaaaaa!!

Muda ulipofika wakaamua kupiga picha ya pamoja ni mshiriki wa VMA YAMORA aliyejishika kwa mbele akiwa na kundi lake wakiwakilisha KASHOZI wakiwa na LUV B mshiriki wa VMA toka KAMACHUMU
Tulishika mbavu na kukaa chini pale VICTORIA COMEDIAN walipopanda katika jukwaa la VMA kutupa rahaaaaa


Alikuwa ni BABA ASIYE NA BABA katikati kutoka kushoto,ambaye aliwakilisha HIP HOP toka kitaa ya HAMUGEMBE ndani ya manispaa ya BUKOBA,yaani ilikuwa ni full shangwe na nyoyo za wana HIP HOP zilisuuzika,yaani ACHAAAAA KABISAAAAAAAAAAA!!!!!! VMA ni balaaaaaaa!

Wanasema msanii ni kioo cha jamii na anaweza kuelimisha jamii kwa kupitia nyimbo zake ,ndivyo alivyofanya RISING STAR wa KAGERA namuongelea SHEMELA kushoto hapo akiimba nyimbo yake mpya iitwayo AFRIKA!!! Full maujumbe humu ndani lakini pia sikiliza VISION FM katika vipindi tofauti utausikia wimbo huu! USIPIMEEE!!
SHEMELA anaendelea kukonga mashabiki wa VMA hapa ni ndani ya ukumbi wa BUKOBA CLUB
RISING STAR toka nchi jirani ya UGANDA nao hawakuwa nyuma,waliamua kuja kusalimia jukwaa la VMA,ilikuwa ni moto wa kuotea mbali!!
Mzee wa ASEKIDO naye alikuwepo akionyesha namna ya kutumia jukwaa kwa nyimbo za asili,ni RISING STAR wa KAGERA mwenye kuchuana vikali na SHEMELA!!! ACHAAAAAAAAAAAAAA KABISAAAAAAAAAAAA!!! Ni nooooooooomaa!
OMMY GUY naye alikuwepo mcheck hapa akishusha verse katika jukwaa la VMA
Katika stage ni picha ya pamoja ya washiriki waliojitokeza katika uzinduzi wa VISION MUSIC AMBASSADOR MEI 19,2013

Baadhi ya mashabiki wakishuhudia vipaji wa wasanii wa KAGERA katika VISION MUSIC AMBASSADOR ndani ya ukumbi wa BUKOBA CLUBA.
Hawa nao ni baadhi yao wakitazama VMA
Mafans wa VISION MUSIC AMBASSADOR wakicheck vipaji!! Achaaaaaaaaaa Kabisaaaaaaaaaaaa!!!!
Mshiriki toka RWAMISHENYE REAL MKUDE naye alikuwepo pia! Anatisha balaaaaaaaa
Toka KAMACHUMU ni LUV B akitoa ya moyoni!!

Hawa ni kaka na dada,lakini wakiwa stejini ni balaaaa!! yaani wanafanya kazi kaka na dada,maskaniiiiiiii

Akiwa na hisia kali ni mwanadada YAMOR mwanachuo wa MUSOMA UTALII akiwakilisha KASHOzI,VISION MUSIC AMBASSADOR,ACHAAAAAAAA KABISAAAAAAAAAA!!!

Monday, 6 May 2013

BUKOBA MAFURIKO BALAA - YAWAACHA WAKAZI WA MJI HUU WAKIWA NNJE YA NYUMBA ZAO







Wakazi wa Omkigusha wakiwa na taharuki mara baada ya maji kuwa mengi na kuingia majumbani mwao na hivyo kusababisha mafuriko yaliyosababisha wakazi hao kukosa mahali pa kulala.....




Sunday, 5 May 2013

MKAZI WA KAGERA TUPE NAFASI UWEZE KUJIACHIA NA VISION FM RADIO 100.0MHz Kibeta,BUKOBA

Wajanja wote wanasikiliza Vision fm radio 100.OMHz kutoka KIBETA, BUKOBA-TANZANIA karibu utusikilize katika msimu huu mpya wa mapinduzi ya utangazaji na masuala mazima yanayohusu burudani hapa Kagera na tuunge mkono kwenye kampeni ya kuinua uchumi na maendeleo ya wana Kagera na hasa Vijana ambao ndio taifa la leo ambalo mara zote wamekuwa na changamoto nyingi za kuanza maisha na kuyafanya kuwa "BORA"

VISION FM RADIO 100.0MHz "ONGEZA MTAZAMO"

TUNAKUKARIBISHA KWENYE SHOW YA VISION MUSIC AMBASSADOR BUKOBA CLUB Tar 19,05,2013 kuanzia saa 8 mpaka saa 12 jioni....


Saturday, 4 May 2013

WAKALI WA MIDUNDO MBALI MBALI MKOANI KAGERA WATAMBIANA KUFUNIKANA VMA








Mtangazaji na Produzer wa Vision fm radio 100.0MHz, Michael Bwoma A.K.A De Marco akiwafanyia interview wasanii ambao tayari wamekubari na kuthibitisha ushiriki wao kwenye show kali ya VISION MUSIC AMBASSADOR (VMA) itakayofanyika jumapili ya tarehe 19,05,2013 katika ukumbi wa Bukoba Club.

Wasanii hawa walifika katika studio za Vision fm radio kuitikia wito wa Tangazo la kuwaita wasanii wachanga na wakongwe ili walete Cds zao na kupata nafasi ya kuwa washiriki na hadi kufikia leo jumamosi ni zaidi ya wanamuziki hamsini wamejitokeza kuweza kujihakikishia nafasi ya kufanya matumbuizo ya VMA kila siku ya jumapili ya mwisho wa mwezi. 

Wasanii hawa wameonekana kuwa wenye hari na kwamba wapo tayari kwaajili ya kufunika katika jukwaa la VISION MUSIC AMBASSADOR… 

Tafadhari usikose kufika siku hiyo kwani kuna mambo mengi yameandaliwa kwaajili yako na kwamba kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kipindi cha THE BASH mara baada ya kuwa kimepikwa upya na kuwa show ambayo itaongoza hapa Mjini Bukoba na Kagera  kwa ujumla..

Thursday, 2 May 2013

HOMA YA JIJI VISION MUSIC AMBASSADOR YA 100.0MHz




Manispaa ya Bukoba haitoshi tena mara baada ya wanamuziki kuwa na hamu ya kufunika na kuonesha kuwa wanaweza kuonesha uwezo wao na kuwapagawisha wapenda burudani wote waliopo mjini humu… kupitia show kali ya Vision Music Ambassador  (VMA) inayoandaliwa na Redio Vision Fm (100.0MHz)
Haya yanatokea ikiwa zimebaki siku chache kwa Vision Fm radio iliyopo Kibeta,Bukoba Tanzania kuandaa jukwaa la kuinua vipaji vya wasanii wa mji wa bukoba pamoja na kagera kwa ujumla ili kuwapa vijana nafasi mpya ya ajira ambayo kwa sasa muziki umewaajiri vijana wengi hapa nchini Tanzania.
Mratibu wa maonyesho hayo Bw. Valerian Rugalabamu amesema kwa upande wa redio ambao ndio waandaaji wakuu wa show  hii wamejipanga vizuri kuwaonesha wakazi wa bukoba wapenda burudani na maendeleo kwa ujumla kwamba kila jambo linawezekana na kwamba Vision fm redio inathamini vipaji vya vijana wa mkoa wa kagera ambao ndio walengwa hasa.