Sunday, 16 March 2014

CCM YASHINDA JIMBO LA KALENGA KWA ASILIMIA 79.4

 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa kumpata Mbunge wa jimbo la Kalenga, baada ya kuzoa kura kwa asilimia 79.4 dhidi ya wapinzani wao Chadema waliopata asilimia 20.1 na Chausta 0.51.

Kwa nafasi hiyo, Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa amekuwa Mbunge mpya akichukua nafasi ya Mbunge aliyefariki jimboni humo, Dr William Mgimwa.

Ushindi wa jimbo la Kalenga, ni mwanzo wa kuanza mbio nyingine za uchaguzi katika jimbo la Chalinze.

CCM wamepata Kura 22908 sawa na asilimia 79.4 ,CHADEMA Wamepata Kura 5800 sawa na asilimia 20.1 na Chausta wamepata kura 143 sawa na asilimia 0.5
 
 
 GODFREY WILLIAM MGIMWA MBUNGE WA JIMBO LA KALENGA ANA UMRI WA MIAKA 32 TU.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.