Vikosi vya usalama
vinavyopambana na magaidi walio ndani ya jengo hilo.
Jeshi la Kenya linasema kuwa limedhibiti jengo hilo ingawa hali bado ni
mbaya
Sehemu ya jengo la Westgate ikitoa moshi
Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa
polisi
Milio
mikubwa ya risasi na milipuko imesikika huku juhudi za usalama zikiendelea
katika jengo la Westgate ambako wanamgmbo wa Al shabaab wameteka jengo hilo
pamoja na wakenya wachache ambao wangali kuokolewa.
Kwa
mujibu wa waziri wa usalama Joseph Ole Lenku, vikosi vya usalama vimeweza
kudhibiti jengo hilo nje na ndani na kwamba ni mateka wachache waliosalia
katika jengo hilo.
Serikali
inasema watu 62 wameuawa lakini shirika la Red Cross lilisema kuwa idadi hiyo
ni 69.
Westgate
ni jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa karibia themanini .
Milio
hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo.
Hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo.
Wapiganaji
wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani.
Walikuwemo
ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati
wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Inaarifiwa
kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Aidha
wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na
kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.
Ripoti
zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika
katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.
Harakati
za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio
ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.
Rais
Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo
na wanamgambo hao.
Helikopta
za polisi zinazunguka juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika
doria. Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru
waathiriwa wakati hali ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.
Awali
jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja
hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya
jengo hilo.
Ripoti
zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia
sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi
ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al
shabaab waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.
Kundi
hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka
majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.