Wednesday, 26 March 2014

WAREMBO WA SOMALIA NA MITINDO YAO





Vijana wa Kisomali wanajulikana kwa urembo wao lakini kwa ajili ya mila na dini yao, hawawezi kushiriki maonyesho ya mitindo ya kisasa kama vile Miss World.

Vijana wa kike na kiume wa Kisomali wameandaa maonyesho ya kwanza ya mitindo ya mavazi katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi. Frenny Jowi alihudhuria maonyesho hayo.

ANTI BARAKA NI MAADUI

 
 Kundi la Anti-Balaka

Mkuu wa vikosi vya Afrika vya kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ,amesema kuwa vijana wa kulinda amani wa kikristo wanaojulikana kama anti-balaka,watatambulika kama maadui kutoka sasa.

Tangazo hilo la Jean -marie Michel Mokoko linajiri baada ya kadhaa za mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya watu 20.

Kundi la Anti-balaka limefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya waislamu baada ya waasi wa kiislamu wa kundi la seleka kuchukua mamlaka mwaka mmoja uliopita.

Jenerali Mokoko pia amelilaumu kundi hilo la anti-balaka kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Afrika vinavyoshirikiana na wenzao wa Ufaransa ili kuzipokonya silaha pande husika.

Mkuu wa kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu Peter Maurer ameanza ziara yake ya siku tatu nchini humo. Kamati hiyo inasema kuwa taifa hilo linakumbwa na janga la kibinaadamu.

Sunday, 16 March 2014

CCM YASHINDA JIMBO LA KALENGA KWA ASILIMIA 79.4

 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa kumpata Mbunge wa jimbo la Kalenga, baada ya kuzoa kura kwa asilimia 79.4 dhidi ya wapinzani wao Chadema waliopata asilimia 20.1 na Chausta 0.51.

Kwa nafasi hiyo, Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa amekuwa Mbunge mpya akichukua nafasi ya Mbunge aliyefariki jimboni humo, Dr William Mgimwa.

Ushindi wa jimbo la Kalenga, ni mwanzo wa kuanza mbio nyingine za uchaguzi katika jimbo la Chalinze.

CCM wamepata Kura 22908 sawa na asilimia 79.4 ,CHADEMA Wamepata Kura 5800 sawa na asilimia 20.1 na Chausta wamepata kura 143 sawa na asilimia 0.5
 
 
 GODFREY WILLIAM MGIMWA MBUNGE WA JIMBO LA KALENGA ANA UMRI WA MIAKA 32 TU.

Saturday, 15 March 2014

WADAU WA AFYA KATIKA PICHA MBALIMBALI TOKA KINGSWAY HOTEL -MOROGORO


Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya Afya hapa mjini Morogoro kings way hotel
Mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro  Dk Godfrey Mtei akiongea na waandishi wa habari katika semina ndani ya ukumbi wa Nkuruma Kingsway hotel  kushoto kwake ni Deo Ngwanansabi toka JHU-TCCP

Dk Isaac Maro toka clouds fm akichangia mada iliyokuwa ikijadiliwa,kulia kwake ni Dk Mosha Aggrey toka JPIEGO na kulia ni Mtangazaji Veronika Mtauka toka Kitulo fm Makete
Dk Martha Kisaga toka Engenderhealth
Dk May Bukuku- JHU-TCCP
Mtangazaji Abbas Mlyuka toka Nuru Fm akiwa na Matrida Leopord toka redio vision fm Bukoba, wakiwasilisha maoni yao kwa waandaaji na watangazaji wa vipindi vya Afya waliokuwa ndani ya semina

Mtangazaji toka Ebony Fm Glory Pelle naye akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa semina

 Mtangazaji toka redio vision Bukoba Matrida Leopord naye akiwasilisha hoja kuhusu masuala ya afya kwa wajumbe

Mtangazaji Khamis Kasapa toka Upland Fm Njombe
Kanuth Dimoso toka JHU-TCCP




 
Somo limenoga hapa ni  Meneja mahusiano Bw. Maurice  Chirimi toka T Marc Tanzania  akidadavua matumizi ya Kondomu kwa wajumbe wa semina hii ya Afya


Monitoring  Manager Bw. Kanuth Dimoso akiwa na Meneja Mawasiliano wote ni kutoka JHU-TCCP Bw. Abu Msemo wakiteta



 
Bi Pamela Kweka toka TCCP akiwasilisha mada kwa wajumbe kuhusiana na Malaria


Tuesday, 11 March 2014

ANGALIA PICHA MBALIMBALI KATIKA SEMINA YA WANAHABARI NA WADAU WA AFYA HAPA MJI KASORO BAHARI( MOROGORO)


Kulia Bi Asia Mohamed toka John hopkins University na Matrida Leopord toka redio vision fm

Hawa ni baadhi ya watangazaji waliokatika semina ya Afya mjini Morogoro iliyoandaliwa na JHU, wa kwanza kushoto ni Debora Mpagama (RFA),Matrida Leopord (Vision Fm),Dk Isaac Maro (Clouds Fm) na Glory (Ebony Fm)

Hawa ni baadhi ya wajumbe katika semina inayoendelea mjini Morogoro hapa Kingsway Hotel